MUNGU,mweza wa yote
*Mmoja Kati ya Watu wa Mungu Walio Wakuu* _Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Luka 1:15._ 📝 Kwenye rekodi ya mbinguni ya walio wakuu, Mwokozi alisema kwamba hakuna aliyesimama aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Kazi aliyokabidhiwa ilikuwa ile ambayo haikuhitaji tu nguvu za kimwili na ustahimilivu, bali pia viwango vya juu vya akili na roho. Maandalizi ya kumkuza sahihi kimwili yalikuwa muhimu sana kiasi kwamba alitumwa malaika mwenye cheo cha juu zaidi mbinguni akiwa na ujumbe wenye maelekezo kwa wazazi wa mtoto. 📝 Jangwani, Yohana alikuwa tayari kujikana mwenyewe na kudhibiti hamu yake ya chakula na kuvaa kwa namna ya usahili wa asili. Vilevile hapakuwa na chochote jangwani pale ambacho kingeondoa mawazo yake kutoka kwenye kutafakari na kuomba. 📝 Shetani aliweza kumfikia Yohana, hata baada yake kufunga kila njia iliyokuwa katika uwezo wake, ambayo Sh...