Posts

MUNGU,mweza wa yote

Image
*Mmoja Kati ya Watu wa Mungu Walio Wakuu* _Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Luka 1:15._ 📝 Kwenye rekodi ya mbinguni ya walio wakuu, Mwokozi alisema kwamba hakuna aliyesimama aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Kazi aliyokabidhiwa ilikuwa ile ambayo haikuhitaji tu nguvu za kimwili na ustahimilivu, bali pia viwango vya juu vya akili na roho. Maandalizi ya kumkuza sahihi kimwili yalikuwa muhimu sana kiasi kwamba alitumwa malaika mwenye cheo cha juu zaidi mbinguni akiwa na ujumbe wenye maelekezo kwa wazazi wa mtoto. 📝 Jangwani, Yohana alikuwa tayari kujikana mwenyewe na kudhibiti hamu yake ya chakula na kuvaa kwa namna ya usahili wa asili. Vilevile hapakuwa na chochote jangwani pale ambacho kingeondoa mawazo yake kutoka kwenye kutafakari na kuomba. 📝 Shetani aliweza kumfikia Yohana, hata baada yake kufunga kila njia iliyokuwa katika uwezo wake, ambayo Sh...

Bucha yenye inzi yafaa kwa kununua nyama,usiogope okoa maisha ya watanzania

Image
By karuti blogu Kuna watu hutumia dawa aina ya FORMALIN ambayo hutumika kutunzia maiti katika kutunzia nyama buchani kufukuza nnzi. Mfamasia mmoja Capt. Kenneth mwanachama wa UPDF, alisema _"ni kweli. Hili ni suala la afya la kitaifa. Baada ya rafiki yake kupoteza mtoto, baada ya uchunguzi kifanyika ikagundulika uwepo wa hiyo kemikali ya formalin katika damu ya mtoto."_ Pale formalin inapokua imeingia mwilini, unaenda moja Kwa moja kwenye ini na kuliharibu. Tafadhali, unapokwenda buchani kununua nyama, ni salama zaidi Kununua nyama ktk bucha lenye nnzi. Tumia uwepo huo kama uthibitisho wa usalama wa nyama isoyokua na kemikali ya  formalin. Kama nyama haina nzi, kinachofanya wasitue juu yake ni uwepo wa formalin. Tafadhali, kua mwangalifu, okoa maisha ya mwingine kama nilivyofanya kwako kwa kushea Kwa mtu wako wa Karibu.

Jinsi ya kutengenenza tomato source

Image
Mara kadhaa nimekuwa nikileta Makala mbalimbali ambazo zinakupa hamasa tu ila Makala ya leo ni pesa mkononi. Pesa mkononi ndiyo ambayo kila mtu anahitaji. Pia nimeamua kukuletea makala haya ili tuendane sawa na Tanzania ya viwanda.  Najua inawezekana kabisa kila mtu kuwa na kiwanda, unashangaa wala usishangae maana huo ndio ukweli maana kila kitu kinapatikana kiurahisi katika mazingira yetu.  Unajua kuwa mikono yako ndiyo itakayokupa pesa? Kama hufahamu basi nimekuja kukujuza ni kivipi utatumia mikono yako ili uweze kuwa tajiri.  Yafuatayo ndiyo mahitaji ya kutengeneza tomato source. 1. Nyanya kilo 1.2. Vitunguu maji viwili.3. Vinegar vijiko 3 vya chai.4. Sukari vijiko 2 vya chai.5. Chumvi kijiko kimoja cha chai6. Maji ya moto kikombe kimoja cha chai.7. Mafuta ya kula vijiko 7 ya vyakula. Haya ndiyo mahitaji ya kutaka kutengeneza tomato souce, hata hivyo kama unataka kutengeneza zaidi ya hapo unatakiwa kuongeza uwiano wa mahitaji hayo.  JINSI YA KUTENGENEZA T...

Ujasiriamali,tujikwamue watanzania

Image
Najua nazungumza na mabilionea wakubwa, kama si mabilionea wa sasa, basi ni mabilionea wa baadaye. Wewe ni bilionea, nakutamkia hili na unatakiwa kuamini pasipo kujali kwamba kwenye akaunti una shilingi elfu moja au chini ya hapo, unachotakiwa kuamini kwamba wewe ni bilionea.  Inawezekana umeanzisha biashara yako, kitu cha ajabu kabisa, fedha hazikai, kila ukipata leo, kesho hazipo, ili kuendesha biashara yako inakupasa kukopa sehemu, ni kweli ulipata faida, ila kwa nini ukope? Kopa wakati ukitafuta mtaji, ila kama umeshafanya biashara na faida ukapata, kwa nini ukope? Kwa nini usitumie faida uliyoipata kukuinua hapo ulipo?  Wengi wanakutana na hali hiyo, si wewe tu, hata mimi nilishawahi kukutana nayo, na si sisi tu, amini hata mabilionea wakubwa walishawahi kukutana na hali hiyo. Hivi unajua ni mabilionea wangapi waliwahi kufilisika? Unamjua Muitaliano Enzo Ferrari? Alipata fedha, akafilisika, akagundua alipofanya makosa, akatafuta tena, akazipata.  Wewe kama binad...

WOKOVU WAREJEA MTWARA

Image
Habari za Leo wapendwa katika BWANA,Natumaini tumeendelea kuwa salama katka mikono ya BWANA huko tuliko!!!Napenda kuwakumbusha kuwa mikutano yetu ya Mtwara i karibu kuanza hivi punde,hivyo kila na tumgeuzie BWANA Nyuso zetu na kuomba sana kwaajili ya wokovu wa wana MTWARA,kwani BWANA aliyeghaili kuwaangamiza Israel kwa maombi ya MUSA,aweza kuwaokoa wana MTWARA kwa maombi yetu ya unyenyekevu NYERERE CAMPUS

Lugha yetu asili yetu,ni lugha ya kiswahili

Image
1. Charger - kimemeshi 2. Remote - kitenzambali 3. Password - nywila 4. Akala (bladder shoes) - kirikiri 5. Passion fruit - karakara 6. Kangaroo - bukunyika 7. Fridge - jokofu 8. Juice - sharubati 9. Chips - vibanzi 10. PHD - uzamifu 11. Masters degree - uzamili 12. Degree - shahada 13. Diploma - stashahada 14. Certificate - astashahada 15. Keyboard - kicharazio 16. Scanner - mdaki 17. Flash disk - diski mweko 18. Mouse (for a computer) - kiteuzi 19. Floppy disk - diski tepetevu 20. Computer virus - mtaliga 21. Distillation - ukenekaji 22. Evaporation - mvukizo 23. Synthesis - uoanishaji 24. Oesophagus - umio 25. Greenhouse - kivungulio 26. Femur - fupaja 27. Germ cell - selizazi 28. Humus - mboji 29. Nector - mbochi/ntwe 30. Nutrients - virutubisho 31. Crystal - fuwele 32. Appetizers - vihamuzi 33. ATM - kiotomotela 34. Business card - kadikazi 35. Scratch card - kadi hela 36. Simcard - kadiwia/mkamimo 37. Memory card - kadi sakima 38. Microwave -...

Hatimaye faru john arejea police DSM.

Image
karuti blogu,kwa ajili yako Askari anayejiita Faru John ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam alikohojiwa na kuruhusiwa kuondoka akaendelee na kazi. Kuripoti kwa askari huyo kunatokana na agizo alilolitoa jana Jumapili, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Peter Sima awe amempeleka leo Jumatatu baada ya kutuhumiwa na wananchi wa Mbagala kwamba amekuwa akidai rushwa. Kamanda Mambosasa pia ametoa wiki moja kwa Kaimu Kamanda Sima awe amefuatilia tuhuma za rushwa zilizowasilishwa kwake na wananchi. Amesema askari huyo ataendelea kufuatiliwa ili kubaini ukweli wa tuhuma zilizotolewa dhidi yake na endapo zitathibitishwa taarifa zitawasilishwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro na atachukuliwa hatua za kisheria. “Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke alimleta huyu askari ambaye nimemuhoji na kumruhusu kuendelea na kazi wakati akiendelea kuchunguzwa ndani ya wiki moja,” amesema Kamanda Mambosasa. Akizung...