Kuzaliwa upya

  1. Mhubiri,mmoja akipokea akiendesha magufuri kule Moscow, urusi Mnamo mwezi machi,1992,alivamiwa ofisini na kijana mmoja mwenye  nguvu  na sura  ya  kutisha. Mhubiri  yule aliogopa, lakini  baada  ya muda mkalimani  wake  alimjulisha  Kuwa  yule kijana  alikuwa  ni mmoja wahalifu  walioshindikana  Moscow. Alikuwa amefungwa  jela Mara nyingi.sasa alikuwa akijisikia hatia na hakuwa na amani.Mhubiri yule  alimsomea 1 yoh.1:9,"Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu  na wa haki  hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote "
   Alimsimulia kisa cha yule  Mwizi msalabani  aliyesamehewa na yesu akiwa juu ya msalaba.Alimhakikishia Kuwa yesu  bado anaokoa  hata  sasa.Anasamehe.Mhubiri alimtia  moyo  yule  kijana  ampokee  Yesu. Yule kijana kijana,huku akitokwa  na machozi, alipiga magoti na kupokea  msamaha  wa  Yesu. 
   Baada ya mwaka mmoja, Mhubiri  yule  alitembelea  tena  Moscow  na kumwona yule  kijana  akimsifu Mungu katika Kwaya.baada ya kumpokea Yesu, alikuwa amebadilika na kubatizwa.
  Ubatizo  ni ishara  ya kuanza maisha mapya. Ni kuzaliwa upya. 
Je, Ubatizo ni wa lazima?
"aaminiye na kubatizwa  ataokoka; asiyeamini,atahukumiwa. " Mk.16:16
Jambo hili  liko wazi. Ubatizo ni moja kati ya mahitaji kwa ajili ya wokovu
  • Siku hizi kuna  Ubatizo  wa  Aina  nyingi. Je, wowote  Kati ya huo si  unakubalika mradi  anayebatizwa  awe  mwaminifu?
"Bwana  mmoja, imani moja, Ubatizo mmoja  "Efe.4:5 Upo mmoja tu  mwingine  ni  wa bandia
  • Je, Yesu alibatizwa  namna  gani? 
"yesu ......akabatizwa  na yohana katika  yordani.mara alipopanda  kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka. " Mk.1:9,10. 
  1. .Mtu anaweza kufanya  nini  Ili abatizwe? 
  1. Kujifunza mapenzi ya Mungu. (Mt.28:19,20).
  2. Kuuamini ukweli wa neno La Mungu (mk. 16:16).
  • 3.Kutubu na kuziacha dhambi zake na kuongoka. (mdo. 3:19).
Maana ya Ubatizo  ni nini? 
  • Ubatizo huonyesha matukio matatu ya mhimu  katika maisha yako muumini  wa  Kweli. 

  1. Kuifia  dhambi 
  2. Kuzaliwa upya katika Kristo na
Kuolewa  na Kristo milele.muungano huo wa kiroho  utazidi  kukomaa na Kuwa  mtamu  zaidi kadri muda  utakavyozidi kwenda  kwa  upendo  utakavyozidi kukua. 
 

Ahsanteni  Sana  kwa  kusoma ujumbe  huu  wa  Kristo  na Mungu  awabariki  woote.Amina.
  

Comments

Popular posts from this blog

Lugha yetu asili yetu,ni lugha ya kiswahili

Okwi sihitaji kiatu cha Dhahabu taarifa zaidi na karuti blogu.

Siku za mwisho zimewadia wapendwa Karibuni tujifunze biblia