Hatimaye ofisa mwingine wa polisi auawa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni ** Ofisa wa Polisi ameuawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kinyerezi Kanga wilayani Ilala. Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni zinasema aliuawa nyumbani kwake. Hata hivyo hakumtaja jina lake. Taarifa zaidi zimesema ofisa huyo wa Polisi alikuwa akifanya kazi wilaya ya Kibaha na alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kigoma hivi karibuni. Kamanda Hamduni amesema taarifa zaidi kuhusu polisi huyo zitatolewa baadaye. “Ni kweli kuna ofisa wa Polisi ameuawa niko eneo la tukio naomba mniache nifanye kazi tutawapa taarifa baadaye,” alisema. Visit  karuti blogu

Comments

Popular posts from this blog

Lugha yetu asili yetu,ni lugha ya kiswahili

Okwi sihitaji kiatu cha Dhahabu taarifa zaidi na karuti blogu.

Siku za mwisho zimewadia wapendwa Karibuni tujifunze biblia