Posts

Showing posts from May, 2017

Chelsea na sunderland Mmmh matatani kwa kosa La kupanga mechi Habari zaidi na karuti dickson

Chelsea wamebeba ubingwa wa mara ya 5 katika ligi kuu, hakika wiki hii ni nzuri kwao na pia kwa kocha wao Antonio Conte kwa kuwa wana jambo kubwa la kujivunia. Lakini sasa Chelsea wameingia matatani baada yakubainika kwamba mchezo wao wa mwisho dhidi ya Sunderland waliupanga kabla ya mchezo kuanza. Sheria za chama cha soka Uingereza zinasema “hairuhusiwi kupanga matokeo, au mashindano au tukio lolote katika mchezo huo kinyume na mipango ya chama cha soka” Sasa wakati wa mchezo kati ya Chelsea na Sunderland, mlinzi mkongwe wa Chelsea John Terry alitolewa uwanjani baada ya kucheza uwanjani kwa dakika 26 tu, swali likaja sub hiyo inatokeaje dakika ambayo ndio namba ya jezi ya Terry? Baada ya filimbi ya mwisho kocha wa Sunderland David Moyes alikiri kwamba kulikuwa na mpango maalum kumuaga Terry ambapo dakika ya 26 wangeufanya mpira usimame ili afanyiwe sub. Chelsea inaonekana walifanya makubaliano na Sunderland kabla ya mchezo huo ili kutekeleza jambo hilo dakika ya 26 namba am...

Magazeti ya siku ya leo 20 may2017

The Sun.Crystal Palace wanaangalia uwezekano wa kuwanunua Bacary Sagna na Gael Clichy ambao wote mikataba yao inakaribia kikomo Manchester City, kinda wa Kisenegal mwenye miaka 18 Mamadou Coulibaly amepata bahati kutoka katika maisha ya ukimbizi hadi kuichezea Juventus. The Sun tena linasema Antonio Conte yuko katika mpango wa kumnunua Pierre Aubemayang ili kuziba pengo la Diego Costa endapo ataondoka Chelsea,na mshambuliaji Ashley Barnes wa Burnley anaweza kujiunga na Crystal Palace au Newcastle ambazo zote zimeonesha kumhitaji. Daily Mail.Claudio Makelele anaweza kupewa nafasi ya kuwepo katika benchi la Swansea baada ya kocha mkuu wa timu hiyo kuamua kuwa na benchi jipya la ufundi, Chelsea na Liverpool zinaweza kumkosa mlinzi wa klabu ya Middlesbrough Ben Gibson baada ya klabu hiyo kusema kuwa hauzwi. Daily Mirror.Manchester United wanapambana vikali kumnunua golikipa Jan Oblak kutokana na kutokuwa na uhakika wa kubaki na David De Gea, huku Crystal Palace nao wameingia kwenye vita y...

Kuzaliwa upya

Mhubiri, mmoja akipokea akiendesha  magufuri kule Moscow, urusi Mnamo mwezi machi,1992,alivamiwa ofisini na kijana mmoja mwenye  nguvu  na sura  ya  kutisha. Mhubiri  yule aliogopa, lakini  baada  ya muda mkalimani  wake  alimjulisha  Kuwa  yule kijana  alikuwa  ni mmoja wahalifu  walioshindikana  Moscow. Alikuwa amefungwa  jela Mara nyingi.sasa alikuwa akijisikia hatia na hakuwa na amani.Mhubiri yule  alimsomea 1 yoh.1:9," Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu  na wa haki  hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote "    Alimsimulia kisa cha yule  Mwizi msalabani  aliyesamehewa na yesu akiwa juu ya msalaba.Alimhakikishia Kuwa yesu  bado anaokoa  hata  sasa.Anasamehe.Mhubiri alimtia  moyo  yule  kijana  ampokee  Yesu. Yule kijana kijana,huku akitokwa  na machozi, alipiga magoti na kupokea  msam...

Tottenham yaichapa Leicester city huku Herry Kane akipiga hatrick

Ni kama waliingia wakiwa na hasira za kukosa kombe ambalo limeenda kwa Chelsea, kwani Tottenham waliingia katika uwanja wa nyumbani wa Leicester City na kutoa kipigo mujarabu. Tottenham wakiongozwa na Harry Kane waliiangamiza Leicester City kipigo cha mabao sita kwa moja huku Kane akiondoka na mpira baada ya kupiga Hattrick na moja la ziada. Kwa hattrick hiyo inamfanya Harry Kane kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tottenham Hotspur kuwahi kufunga hattrick nne katika msimu mmoja tangia Jimmy Greaves afanye hivyo mwaka 1969. Mabao hayo manne ya Harry Kane yamempeleka hadi katika kilele cha ufungaji bora msimu huu kwa kufikisha mabao 24 na kumpita Romelu Lukaku aliye na mabao 23. Magoli mengine ya Tottenham Hotspur yaliwekwa kimiani na Heung Min Son aliyefunga mawili, huku lile la kufutia machozi la Leicester City likiwekwa kimiani na Ben Chilwell. Lakini matokeo hayo hayabadilishi mbio za ubingwa wa Uingereza kwani tayari bingwa ameshapatikana ila yanawasaidia tu Tottenham kuongeza idadi ya ...

Hatimae malalamiko ya Simba yafikishwa FIFA kwa madai ya kupokonywa pointi 3

Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema, tayari wametuma malalamiko yao FIFA kuhusu pointi tatu walizonyang’anywa na TFF baada ya Kagera Sugar kumtumia mchezaji Mohamed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano walipocheza dhidi mechi ya ligi dhidi ya timu hiyo ya Bukoba. Kaburu amesema barua yao ya malalamiko imepokelewa na FIFA na wanachosubiri ni kusikia uamuzi gani utatolewa na shirikisho hilo la soka Duniani. “Tumeshatuma malalamiko yetu na yamepokelewa FIFA, tumeainisha tunataka nini. Nisiwasemee, wao watasoma na wataamua halafu watatujulisha walichokiamua,” amesema Kaburu wakati akizungumza na Clouds FM kupitia kipindi cha michezo Sports Extra. Simba walifikia uamuzi wa kupeleka jambo hilo FIFA baada ya Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za wachezaji kutengua uamuzi wa Kamati ya saa 72 ambayo awali iliipa Simba pointi tatu na magoli matatu baada ya kubaini ni kweli Kagera Sugar ilimchezesha Fakhi dhidi ya Simba huku akiwa na kad...

Vijana wanaosakata kabumbu zuri kabisa (Serengeti boys U17)wamepata ushindi ambao unawaweka Sehemu Nzuri Sana baada ya kufikisha point 4 #taarifa na karuti dickson

Serengeti Boys imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya AFCON U17 baada ya kuifunga Angola kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa Kundi B uliochezwa jioni ya leo Alhamini Mei 18, 2017. Vijana wa Serengeti Boys ndio walikua wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya sita kipindi cha kwanza baada ya Kelvin Naftal kupasia kamba kwa kichwa akiunganisha krosi ya Nickson Kibabage .  Dakika ya 18 Angola walisawazisha bao hilo kupitia kwa Pedro baada ya kutumia vizuri makosa ya safu ya ulinzi ya Serengeti Boys na kufanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare kwa kufungana 1-1. Kipindi cha pili Serengeti waliongeza kasi kutafuta bao na kufanikiwa kufunga dakika ya 69 mfungaji akiwa ni Abdul Suleiman baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Yohana Mkomola .  Serengeti Boys imefikisha pointi 4 baada ya kupata pointi moja kwenye mchezo wa kwanza kufuatia kutoka sare ya bila kufungana dh...

Siku za mwisho zimewadia wapendwa Karibuni tujifunze biblia

Halleluya  karibuni ndugu  Zangu  wapendwa  kwenye  ukrasa  wangu  ili  tujifunze  neno  La BWANA kutoka kwa ndugu. Lawrence odondi   Kuna mambo  tunatakiwa  kuyafahamu  kwa siku  hizi  za mwisho  Hivyo basi  yatupasa  tujiandae  ili  tuweze  kushinda  vita  hii  ambayo  Kristo  alishaianza  lakini  tumaini  tumepewa tumaini  rejerea Maombolezo  2:19 ni kwa Maombi  tu  utapata  kushinda Lakini  Licha  ya hayo  yote  mtunga  zaburi  anatukumbusha  ni nini  Mimi  na wewe  tufanye  ili  tuyashinde  yote  zaburi 119:9-11 Kumbe basi  ukimkaribisha  Mungu  katika  maisha  yako  hatoweza  kushindwa  hata  iwe  vita  ya  namna  gani  Mpendwa  kwa siku  ya  L...

Majibu ya waziri mwigulu kuhusu fomu za pf3,taarifa zaidi na karuti blogu

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi , Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuanzia sasa mtu yoyote atayeweza kupata majeraha yasiyokuwa na utata wapewe matibabu kwanza hospitali bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Jeshi la Polisi (PF3) kama ilivyozoeleka . Mwigulu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook kwa kusema utaratibu huo unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vya usalama ili kubaini ukweli wa jeraha la muhusika. "Tumeamua majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka na mtu mwenye majeraha yasiyo na utata wapewe matibabu kwanza bila PF3..Hatua za kufuata PF3 zianze mara moja wakati akiendelea kupewa matibabu, hii tunalengea kuokoa maisha yao kwanza, utaratibu huu unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vyetu vya usalama ili kubaini ukweli jeraha la mhusika". Ameandika Mwigulu Mwigulu amesema hayo baada ya Jeshi la Polisi kutupiwa lawama nyingi kutoka kwa wananchi walipatwa na matatizo kushindwa kupewa huduma hospitali kwa har...

Hatimaye ofisa mwingine wa polisi auawa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala , Salum Hamduni ** Ofisa wa Polisi ameuawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la Kinyerezi Kanga wilayani Ilala . Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala , Salum Hamduni zinasema aliuawa nyumbani kwake . Hata hivyo hakumtaja jina lake. Taarifa zaidi zimesema ofisa huyo wa Polisi alikuwa akifanya kazi wilaya ya Kibaha na alikuwa amehamishiwa mkoa wa Kigoma hivi karibuni. Kamanda Hamduni amesema taarifa zaidi kuhusu polisi huyo zitatolewa baadaye. “Ni kweli kuna ofisa wa Polisi ameuawa niko eneo la tukio naomba mniache nifanye kazi tutawapa taarifa baadaye ,” alisema . Visit  karuti blogu

Karuti tayari ameanzisha blog

Karbuni nyote